Fasihi Simulizi Gredi 10
KShs 920.00
Upeo wa Marejeleo ya Fasihi Simulizi, Kitabu cha Marejeleo kwa
Gredi za 10-12 ni kitabu kilichoandikwa kwa upeo mpana wa kitaaluma
na ubunifu wa hali ya juu. Kimeandaliwa ili kutosheleza kikamilifu
mahitaji ya Mtaala wa Kiumilisi katika ngazi ya Shule ya Sinia, kikilenga
kukuza uelewa wa kina wa fasihi simulizi kama nguzo ya utamaduni na
maarifa ya kijamii.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaompa mwanafunzi uhuru wa
kujifunza, kutafakari na kufanya marejeleo binafsi, huku kikisisitiza
ukuzaji wa umilisi kama vile uchambuzi wa kina wa fasihi simulizi.
Kitabu cha Marejeleo ya Fasihi Simulizi (Gredi 10–12) kinachambua kwa
kina tanzu mbalimbali za fasihi simulizi kama vile hadithi, maigizo,
mazungumzo, semi, na mashairi.
Mada zimepangwa kwa mtiririko unaoendana na mtaala
uliopendekezwa huku kila utanzu ukiwasilishwa kwa maelezo
yanayofaa kwa marejeleo na utafiti. Maelezo haya yatamwezesha
mwanafunzi kuelewa dhima, maudhui, muundo na umuhimu wa fasihi
simulizi katika jamii.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na waandishi
wenye uzoefu mpana katika taaluma ya Kiswahili na uandishi wa vitabu
vya kiada na ni hazina muhimu kwa maarifa ya kitaaluma, stadi na
utafiti katika fasihi simulizi.






