Skip links

Kiswahili Grade 10

Kiswahili Grade 10

KShs 920.00

Akili Pevu Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 10 ni kitabu
kilichoandikwa kwa ubunifu mkuu. Kimetimiza na kutosheleza mahitaji yote
ya Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaomwegemea
mwanafunzi zaidi na kinakuza umilisi unaotolewa na mtaala.
Katika utunzi wake, kitabu hiki kinampa mwanafunzi nafasi zaidi na kumfanya
mwalimu kuwa mwelekezi tu bali si mtoaji wa elimu.
Kitabu hiki kimezingatia mambo muhimu yafuatayo.
• Ni kitabu cha kipekee kilichotumia lugha sahili inayoeleweka kwa urahisi
na mwanafunzi wa Gredi ya Kumi.
• Mada zimepangwa kulingana na mpangilio uliopendekezwa na KICD. Kila
suala kuu linaanza kwa picha ya kusisimua inayompa mwanafunzi hamu
ya kujifunza.
• Shughuli anuwai za kipekee zinazokuza stadi nyingi za kufikiria kama vile:
kuchanganua, kueleza, kutambua, kutafiti, kubainisha na hata kuhakiki.
• Kimehusisha shughuli mbalimbali za ujifunzaji katika kila mada ndogo;
shughuli hizi zinawashirikisha wanafunzi wakiwa wawiliwawili, kwenye
vikundi na akiwa peke yake.
• Mwongozo wa mwalimu unaotoa maelekezo dhahiri kwa mwalimu kuhusu
namna ya kushughulikia vipindi na shughuli katika kila mada.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa utaalamu na waandishi wenye uzoefu mwingi
katika uandishi wa vitabu vya kiada.

1
    1
    Your Cart
    Essential Maths Grade 10
    1 X KShs 920.00 = KShs 920.00
    × Whatsapp